News / Local News / Askari usalama amvaa mwendesha baiskeli

image

Askari usalama amvaa mwendesha baiskeli

By Editor

Polisi wa kikosi cha usalama barabarani akipambana na mwendesha baiskeli aliyedaiwa kukaidi amri na maelekezo ya usalama barabarani katika eneo la Mbuyuni Kinondoni jijini Dar es Salaam leo asubuhi. PICHA: ROMI
image

image

Rapsha imeibuka leo asubuhi katika eneo la Mbuyuni kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi Kinondoni jijini Dar es Salaam, baada ya mwendesha baiskeli kukaidi amri ya askari wa usalama barabarani, hali iliyopelekea askari huyo kumvaa na kutaka kumnyang’anya baiskeli yake.

Askari huyo alichukua hatua ya kuivuta baiskeli hiyo pembeni kuchukua hatua zaidi, baada ya mtumiaji huyo wa barabara kukosa kufuata maelekezo ya yaliyokuwa yaitolewa katika kudumisha utaratibu na usalama barabarani.

Hadi kamera yetu inaondoka katika eneo la tukio, askari huyo alikuwa akifanya mahojiano na mtuhumiwa na kupanga namna ya kuchukua hatua zinazofaa kwa lengo la kudhibiti uhalifu wa jinsi hiyo barabarani.


 
image
image
This text will be replaced
image