News / Sports / Bongo Movie waitandika Kadanse FC

image

Bongo Movie waitandika Kadanse FC

By manny

Mtanange wa kukata na shoka kati ya wasanii wa Filamu (Bongo Movies FC) na Kadanse FC Uliofanyika Jana maalumu kuchangia waathirika wa Mafuriko yaliyotokea Mwaka Jana ulimalizika kwa wasanii wa Filamu nchini kuitandika Kadanse FC jumla ya mabao 4 - 3.

Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na viongozi wa juu kabisa katika serikali na washabiki wengi waliojaza uwanja mkuu wa Taifa.

Ilikuwa ni Mechi maalumu ya kuchangia Wahanga wa Mafuriko lakini iliyokuwa ya kukata na shoka ambapo timu zote zilionyesha Soka la hali ya Juu.

Bongo Movie ndiyo walikuwa wa Kwanza kujipatia bao kunako Dakika ya 15 ya mchezo lilofungwa na Dr Cheni.

Mabao mengine ya Bongo Movie yalifungwa na Ray, Rich Mtambalike pamoja Steve Nyerere.

Akiwashukuru wacheza Filamu hao kwa jitihada zao za kuwa karibu na Wananchi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik alisema kitendo walichofanya wasanii hao ni cha kuigwa na wengine kwani wameguswa na yaliyotokea.

"Hawa waliopatwa na Janga hili sio ndugu zao, lakini kwasababu ya mioyo yao ya huruma juu ya Watanzania wenzao ndiyo sababu ya kuandaa kitu kama hiki ambacho kwa namna moja ama nyingine wanawasaidia ndugu zao" alisema Meck Sadik

Bongo Movies walikabidhiwa Kikombe chao na Mkuu wa Mkoa mara baada ya Mtanange huo.

image
image
This text will be replaced
image