News / Local News / Foleni sasa yaingia viwanja vya ndege

image

Foleni sasa yaingia viwanja vya ndege

By Editor

Wasafiri wakipanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika terminal ya zamani. PICHa: ROMI image

image

Wakati Serikali ikihaha kukabili tatizo sugu la foleni za barabarani katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo mengine ya miji mikoani, hali pia imeendelea kuwa tete katika viwanja vya ndege vya usafiri wa anga, ambapo sasa abiria wanashindwa kupata usafiri wa kuaminika.

Hali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere imeelezwa kuwa matatizo kutokana na kiwanja hicho kuwa na wageni wengi hususani kutoka nje ya nchi wanaokuja kwa utalii, lakini udogo wa kiwanja hicho unalazimika kukatisha au kusubirisha safari nyingine, na kupelekea Taifa kukosa mapato hasa watalii wanaposhindwa kuja kwa wingi kwa kikwazo cha usafiri.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini Suleiman Suleiman uwanja huo kwa sasa ni mdogo na unatakiwa kupanuliwa ili kuwezesha usafiri wa abiria kwa njia ya anga uwe wa kuaminika.

Kiongozi huyo aliwahi kuwaeleza wanahabari kwamba mamlaka za viwanja vya ndege zina mkakati wa kupanua uwanja huo kwa kuongeza terminal ya tatu, katika zioezi litakaloanza Mwezi Marchi mwaka huu.

Upanuzi wa uwanja huo unategemewa kuliwezesha Taifa kumudu ongezeko
kubwa la watalii wanaotembelea mbuga zetu za wanyama na vivutio vinginen katika kuingiza kipato kikubwa kwa Taifa na kuleta tija katika sekta hiyo.

Kwa sasa utalii unakabiliwa na changamoto nyingi mojawapo usafiri wa kutoaminika.

 
image
image
This text will be replaced
image