Hali ya barabara kuu jijini
Magari yakiwa kwenye foleni katika barabara ta Ali hassan Mwinyi eneo la Bamaga karibu na kituo cha televisheni cha TBC jijini Dar es salaam. PICHA: ROMI


Msongamano wa magari umeendeelea kuwakabili wasafiri katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam, ambapo katika eneo la Bamaga kamera yetu ilikumbana na dhahma hiyo na kulazimika kumulika tena tatizo hilo linaloonekana kuzoeleka na watumiaji sasa.
Licha ya wadau mbalimbali wakiwemo Benki ya Dunia kutoa ushauri na mbinu za kumaliza msongamano huo, bado utekelezaji wake umeishia kapuni katika wakati ambao Taifa na wananchi wake wanaendelea kupoteza kipato kutokana na kikwazo cha usafiri duni.
Hapo awali mwanzoni mwa mwaka huu, waziri mwenye dhamana na ujenzi wa barabara Mhe John Pombe Magufuli alitangaza kuwepo mkakati wa upanuzi wa barabara hiyo kutokea Mwenge hadi katika eneo la Morocco, mpango ambao bado haijabainika utaanza kufanya kazi wakati gani.
Top Stories »





