Huduma za kijamii Ngorongoro zaimarika
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Embaraway wakiwa wanamsikiliza walimudarasani. PICHA: ROMI 

Kufuatia mchango wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mbuga ya Taifa Ngorongoro kusaidia jamii zinazozunguka mbuga hiyo, matunda yameanza kujitokeza baada ya wanafunzi kuhudhuria madarasani kwa elimu, kutokana na upatikanaji wa madarasa na waalimu.
Wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakinufaika kwa huduma za elimu, afya na maji kupitia miradi mbalimbali ya Serikali, ikichagizwa na mchango wa hifadhi ya Ngorongoro.
Hivi karibuni hifadhi hiyo ilielezwa pia kutoa ushauri wa jinsi jamii hiyo ya kifugaji inavyoweza kupunguza idadi ya mifugo kwa kufuga kisasa, ili kuepusha uharibifu wa mazingira, kuhamahama na kuvamia maeneo ya mbuga.
Jamii hiyo kadhalika kwa mujibu wa mamlaka hiyo, imekuwa ikipatia nyenzo za ufugaji kama mbegu za majani ya kulishia mifugo pamoja na majosho.
Top Stories »





