Kamati Dodoma yakaa kujadili usalama
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi (kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Dodoma leo. Kulia ni makamu mwenyekiti wa kikao hicho na Mbunge wa Chironoa Hezekiah Chibulunje. PICHA: ROMI


Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe Dkt Rehema Nchimbi ameongoza wajumbe wa Kamati ya ushauri ya mkoa huo katika kikao cha kujadili masuala nyeti yanayohusu usalama wa wananchi dhidi ya vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa amani mkoani humo.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa Dkt Nchimbi, masuala kadha yamejadiliwa katika Nyanja ya usalama katika kuhadikisha utulivu na amani unadumishwa ndani ya mkoa huo.
Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na mbunge wa jimbo la Chironoa Mhe Hezekiah Chibulunje,kadhalika suala la miradi ya maendeleo nalo limegusiwa na kujadiliwa kwa kina katika kikao hicho, ambapo kamati hiyo imetazama ni kwa jinsi gani miradio hiyo imetekelezwa kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye maeneo yaliyolengwa.
Top Stories »





