News / Politics / Kesi ya Kawe yafutwa, Mbatia akubali yaishe

image

Kesi ya Kawe yafutwa, Mbatia akubali yaishe

By Editor

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Silaa (kushoto) na Katibu Mkuu wa
NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza wakikumbatiana baada ya kukubaliana
kufutwa kwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania ambapo Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa James
Mabata alimlalamikia mshindi Halima
Mdee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kwa kufanya kampeni chafu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka
2010 kwenye kinyang;anyiro cha Ubunge jimboni Kawe.
PICHA:ROMI
image

image

Mahakama kuu nchini imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili mbunge mteule wa jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam kupitia CHADEMA Halima Mdee, kufuatia mashitaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo na aliyekuwa mpinzani wake kutoka chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia, kwamba alifanya kampeni chafu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Baada ya mazungumzo marefu baina ya pande hizo mbili (CHADEMA na NCCR Mageuzi) jijini Dar es Salaam, hatimaye makubaliano yalifikiwa kwa makatibu wakuu wa vyama hivyo kuafiki kwa kauli moja kufuta kesi hiyo mahakamani.
Wakidhihirisha kumaliza sakata hilo, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbroad Slaa alilakiwa kwa furaha na mwenzake kutoka Chama Cha NCCR Mageuzi Samwel Ruhuza, kueleza kufikia tamati kwa ugomvi huo ambao umedumu kwa takribani mwaka mmoja sasa.
Itakumbukwa mara tu baada ya mgombea Halima Mdee kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Octoba mwaka 2010 jimboni Kawe, aliyekuwa mpinzani wake wa Karibu na mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa James Mbatia alifikisha malalamiko yake mahakamani, kupinga kile kilichoelezwa ni kampeni chafu zilizoendeshwa na mshindi wa kiti hicho, na kuhujumu kikatiba nafasi yake ya kujipatia ushindi kwenye king’ang’anyiro hicho.

 
image
image
This text will be replaced
image