Kiama cha Wakenya ICC Kenyata, Ruto kitanzini
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa katika Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai ICC, ambapo jopo la majaji walioendesha mashtaka dhidi ya Wakenya sita, wanaoshukiwa kuwa vinara wa machafuko ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo limesoma hukumu, kwa kuwakuta washitakiwa wanne kuwa na kesi ya kujibu. 

ICC inayoongozwa na jaji Luis Morano Occampo, ilijitwisha jukumu la kuchunguza na kuendesha mashitaka hayo kufuatia mauaji mabaya yaliyolighubika Taifa hilo jirani, baada ya king’ang’anyiro cha uchaguzi wa tarehe 30 Desemba mwaka 2007.
Akisoma ripoti hiyo ya uchunguzi ya ICC, jaji Catherine Theodoflova amesema walikutwa na hatia ya kusimama kizimbani ni pamoja na wanasiasa wakongwe wanaochachafya na kampeni za kugombea uraisi mwaka huu Uhuru Kenyata na mwenzake William Rutto, pamoja na mwandishi Joshua Sang na mbunge Francis Muthaura.
Aidha washitakiwa wengine Hendry Kosgei na Hussein Ally wameondolewa katika rungu hilo, kwa kile kilichobainishwa kuwa wamekosa ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani, hivyo wameachiliwa huru.
Uamuzi huo uliosomwa majira ya mchana leo, umeonekana kuwashtua Wakenya wengi kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, katika wakati ambao Taifa hilo limekuwa kwenye hali ya sintofahamu kuhusiana na maamuzi ya mwisho ya ICC.
Imearifiwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita Uhuru Kenyata na William Rutto wamekuwa wakipiga kampeni, wakijiandaa katika uchaguzi mkuu ujao kwenye kugombea nafasi ya uraisi.
Top Stories »





