News / Local News / Bilali adadisi usalama wa wafanyakazi migodini

image

Bilali adadisi usalama wa wafanyakazi migodini

By Editor

Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilali, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Usalama Kazini, Nassor Abdallah, katika kampuni ya uchimbaji madini ya Manta kwenye mradi wa mto Mkuju mkoani Ruvuma. PICHA: ROMI
image

image

Ziara ya Makamu wa Raisi wa nchi Dkt Mohamed Gharib Bilali mkoani Ruvuma, imeshuhudia mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa migodini, ambapo alitaka kupata maelezo ya kina ya jinsi wananchi hao wanavyolindwa kutokana madhara, hususani kwa kuwa na vifaa stahiki vya kufanyia kazi.

Katika ziara hiyo, uongozi wa kampuni ya Manta Tanzania ulimwonyesha vifaa vya usalama kazini vinavyotumika na wafanyakazi wa migodini wanapokuwa kwenye maeneo ya kazi.

Kampuni ya Manta Tanzania imepata tenda ya kuchimba madini aina ya Uraneum katika mradi maalumu unaoendeshwa katika eneo la mto Mkuju mkoani Ruvuma.

Hata hivyo wafanyakazi wengi nchini wanaopata fursa ya kutokea katika vyombo vya habari, wamekuwa wakibainisha madhara lukuki wanayoyapata kutokana na sumu za viwandani na migodini, ambayo aghalabu yanatokana na kutokuwa na vifaa stahiki vya kazi, na mara nyingi wamiliki wa migodi na viwanda huwatelekeza bila fidia wala matibabu yanayofaa mara wanapokumbwa na magonjwa.

 
image
image
This text will be replaced
image