Mbunge amkabidhi mlemavu msaada wa kiti
Mwananchi mwenye ulemevu wa viungo akisukumwa na Mbunge wa Viti maalumu Ritta Kabati (katikati) baada ya kumkabidhi msaada wa kiti mjini Iringa. PICHA: ROMI


Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi CCM Mhe Ritta Kabati amemzawadia mwananchi mwenye ulemavu wa viungo kiti chenye magurudumu cha kusukuma, katika makabidhiano ya msaada huo yaliyofanyika leo mjini Iringa.
Mhe Kabati ametoa msaada huo katika moja ya ziara zake kwenye eneo la mjini Iringa, alipotembelea kujua matatizo yanayowakabili wananchi.
Wabunge wa viti maalumu wamekuwa wakishutumiwa kutojitokeza kikamilifu katika kushughulikia matatizo ya wananchi moja kwa moja, suala ambalo wengi wa wabunge hao wamepinga na kueleza wanachapa kazi sawa na wabunge wa kuchaguliwa.
Top Stories »





