Mr Blue afukuzwa kundini, kutinga mahakamani
Mmomonyoko katika makundi ya Wanamuziki wa kizazi kipya nchini Bongo Flavor umeendelea kukisakama kizazi hicho, baada ya kundi la ‘Micharazo’ kutangaza kumuengua kundini nyota wake mahihiri Heri Sameer Rajab maarufu kama Mr Blue kutokana na utomvu wa nidhamu. 

Taarifa kutoka ‘Micharazo’ imeeleza kwamba licha ya msanii huyo kutimuliwa, hali kadhalika ammepewa katazo la kutotumia nembo yoyote ya kampuni hiyo au jina la kundi hilo (Micharazo) katika nyimbo au albamu zake.
“Tumemuengua, tumemvua gamba la Micharazo… na ataingia kwenye mikono ya sheria” amesema mmoja wa viongozi wa kundi hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Kiongozi huyo ameongeza kwamba sheria iliyomg’oa nyota huyo haiko kwa ajili yake tu, bali ni kwa mtu yeyote anayekwenda kinyume cha sheria zilizotungwa na kukubaliwa na wanakundi wote.
“Si Blue tu! Mtu yeyote ataingia kwenye mikono ya sheria kama atatumia vibaya nafasi yake kwenye kundi” amesema kiongozi huyo na kuongeza kwamba ubinafsi ni sumu na haupaswi kupewa nafasi.
Imeelezwa kuwa miongoni mwa makosa ya msanii huyo ni kuimba kwa kushirikisha wasanii wadogo (underground) kutoka nje, badala ya kukuza wale walioko ndani ya kundi, na kwamba tukio hilo linalea ubinafsi ndani ya kundi.
Top Stories »





