Mwakyembe ammaliza Mganda kwa pointi 99
Hatimaye vuta nikuvute baina ya wanamasumbwi Benson Mwakyembe kutoka Mbeya Tanzania na Mustapha Katende kutoka nchini Uganda imekwisha, baada ya Mwakyembe kufunga mwaka kwa kumtandika Mganda huyo kwa pointi 99 dhidi 94 mjini Songea jana jioni. 

Bondia huyo mwenye rekondi nzuri katika siku za hivi karibuni, ametawazwa bingwa wa mchezo huo wa uzito wa Kati kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, baada ya kutawala mpambano huo kutoka mwanzo hadi mwisho na kuimarisha mashambulizi katika dakika za mwisho hali iliyopelekea ushindi huo.
Mpambano huo uliopigwa katika mji wa Songea Ruvuma, umemaliza ubishi wa muda mrefu baina ya mabondia hao ambao kwa nyakati tofauti kila mmoja alitamba kummaliza mwenzake.
Akishangiliwa kwa shangwe kutoka mwanzo hadi mwisho wa mchezo, Mwakyembe aliongeza nguvu na kupata ari ya kumsogeza katika hatua ya ushindi pale alipokuwa akikumbana na sauti za mashabiki kila aliporusha mkono.
Top Stories »





