News / Entertainment / Mwakyembe kuzichapa na Mganda Boxing Day

image

Mwakyembe kuzichapa na Mganda Boxing Day

By dar411

Bondia mashuhuri nchini hususani ukanda wa nyanda za juu Kusini Benson Mwakyembe, anatarajiwa kupanda ulingoni Desemba 26 wiki ijayo kumvaa mwanamasumbwi kutoka Uganda Mustapha Katende, katika mchuano Super Middle Weight. image

image

Akitangaza maandalizi ya mchuano huo, Katibu mkuu wa Shirikisho la Ngumi za kulipwa nchini Yasin Abdallah Ustaadh amebainisha kuwa mpambano huo utapigwa katika mji wa Songea, na kwamba maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa cha 95%.
Ameongeza kuwa mabondia wote tayari wako katika hali ya kimazoezi na kuwa watapima uzito tarehe 25 siku ya Krismasi, katika eneo la Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mjini Songea.
Mpambano huo ulioelezwa kuwa wa 13 na wa mwisho kwa mwaka huu katika Shirikisho la ngumi nchini, utawahusisha mabondia hao katika hali iliyoelezwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana na historia ya hivi karibuni ya wachezaji wote wawili.


 
image
image
This text will be replaced
image