News / Articles / Nini hatma ya ongezeko la joto duniani?

image

Nini hatma ya ongezeko la joto duniani?

By dar411

Je, uhai utapotea duniani na uso wa ardhi kubakia miamba na udongo pekee? au tutaweza kuidhibiti hali hii? Je, hatua zinazochukuliwa hivi sasa zinaweza kupingana na wimbi la mabadiliko haya yenye mchanganyiko wa asili (nature) na uharibifu wa binadamu (human distruction) duniani? image

image

Inakadiriwa kuwa joto katika uso wa dunia liliongezeka kutoka nyuzijoto 0.3 (Centigrade) hadi kufikia 0.6, katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, na kwa mujibu wa tafiti za kisayansi ongezeko hilo katika karne ya 21 litafikia nyuzi 2 hadi 3.5 na zaidi ya hapo kwa miaka ijayo.
Hii inatokana na ripoti ya utafiti ya pamoja iliyotolewa na jopo la zaidi ya Wanasayansi 1,000 waliojumuika katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (Climate Change) mwaka 1995.
Haya, si matokeo ya kubeza kwani kwa mujibu wa tafiti hizo, hata katika enzi za theluji (Ice Age) maelfu ya miaka iliyopita, wastani wa joto ulikuwa nyuzi joto 3 – 6 pekee chini ya wastani wa sasa, lakini mazingira na theluji yake viliendelea kubadilika hadi kufikia hali iliyopo sasa.
Hali kadhalika, ongezeko la digrii 2, litaweza kusababisha kupanda kwa kina cha maji ya bahari kuanzia cm 15 kwa uchache hadi cm 95, kwa mujibu wa Tasisi ya Kimataifa ya Mazingira “Grave Impact of Global Warming”
Ongezeko la joto linatokana na nini? Kiasili mabadiliko ya hali ya hewa hutokea katika sura mbili, ya kwanza ni ile ya kuongezeka kwa joto (heating effects) na ya pili ni kupungua (cooling effects), na hii imekuwa ikifanyika polepole kwa miaka mingi na kwa hali tofauti.
Ongezeko linaweza kutokana na mabadiliko ya kiasi cha joto linalotoka kwenye jua na kupokelewa katika uso wa ardhi, pili ongezeko la hewa ya carbon hasa kwa kuchagizwa na kuunguzwa kwa mafuta ya nishati viwandani na mashine mbalimbali huruhusu miale ya jua kuuufikia uso wa dunia moja kwa moja baada ya kudhoofisha tabaka linalokinga miale hiyo (ozon layer)
Aidha, baada ya uso wa dunia kupokea joto hilo, pia hewa ya carbon (natural oxides of carbon) huzuia mtawanyiko wa joto hilo kwenda angani, na hivyo kusababisha joto kugandamana kuzunguka dunia na kupelekea kuungua zaidi kwa uso wa ardi pamoja na bahari (heating effects).
Kwa upande wa pili, chembechembe za vumbi linalotokana na milipuko ya volcano zilizovukishwa angani na kutanda kwa miaka mingi hufanya kazi ya kutawanya miale ya jua hivyo kuipunguza isifike kwa wingi katika uso wa dunia (cooling effects).
Hali kadhalika shughuli za viwanda na kilimo huweza pia kutawanya angani chembechembe za vumbi la mazao ya kilimo, ambalo nalo hutanda na kuunda tabaka linalochangia kupunguza nguvu ya miale ya jua.
Imebainika kuwa iwapo jitihada mahususi zinazopigiwa upatu duniani kote zitafanyiwa kazi, huenda tatizo hilo la ongezeko likapunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Changamoto kubwa bado inabaki; kutokana na kuendelea kukua kwa teknolojia, katika wakati ambao kila nchi inajitahidi kukuza uchumi wake na kuwawezesha wananchi wake, na upande wa teknolojia hiyo ukiendelea kuhitaji nishati na nguvu zinazochafua mazingira, ni nani atakubali kupunguza uzalishaji kwa manufaa ya mazingira?
Uzalishaji wa viwanda hasa katika nchi tajiri kama Marekani, Ulaya na China ndio wanaochangia vikubwa hewa ya ukaa inayoteketeza tabaka la ozon, na wengine wakiwa nyuma kuchangia uharibifu huo kama vile Brazil, Mashariki ya Kati na nchi nyingine za ulimwengu wa tatu.
Mafanikio mazuri yatakuja, na salama ya kizazi kijacho itadhihirika iwapo Mataifa yote kwa pamoja na kila mtu ataweka dhamira wazi ya kuchangia jitihada hizi kwa kuongeza zaidi upandaji miti, na kuepuka ukataji, kupunguza matumizi ya mashine, mitambo na injini zinazotumia mafuta ya kuunguza pamoja hali nyingine zozote hatarishi kwa hali ya hewa.

 
image
image
This text will be replaced
image