News / Articles / Polisi chanzo cha kuvusha magendo mipakani

image

Polisi chanzo cha kuvusha magendo mipakani

By dar411

Wakati Serikali ikitaka ulinzi kuimarishwa katika maeneo ya mipaka na kuzuia mazao kama sukari na mahindi yasivushwe kwenda nchi jirani, Jeshi la Polisi limelaumiwa kwa rushwa na kufanya urasimu kwenye vituo vya ukaguzi, hivyo kuzidisha kadhia hiyo. image

image

Akizungumzia hali katika mpaka baina ya Kenya na Tanzania katika eneo la Sirari mkoani Mara, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Tarime Amos Sagara, ameeleza kuwa hali hiyo imefanya biashara za mipakani kuwa ngumu.
Amesema urasimu unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuweka vizuizi vingi dhidi ya magari na wakati mwingine kuwasimamisha kwa muda mrefu na kudai faini za kila aina, kunazua usumbufu unaowashawishi wafanyabiashara kuamua kutumia njia za panya.
Aidha kiongozi huyo amefafanua kuwa hali hiyo inakwenda kinyume na utaratibu mpya wa kibiashara baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na unazorotesha ukuaji wa shughuli za kibiashara.
Imebainika kuwa, bidhaa nyingi sasa haziingii wala kuvuka mipaka kupitia vituo stahiki vilivyopangwa, na badala yake wafanyabiashara wengi wamelazimika kutumia njia za magendo kukwepa kadhia ya usumbufu mipakani na kueleza kutonufaika na kazi hizo.

 
image
image
This text will be replaced
image