News / Articles / Polisi kufutiwa kodi, waalimu,madaktari nao wafikiriwe

image

Polisi kufutiwa kodi, waalimu,madaktari nao wafikiriwe

By dar411

Imezoeleka kusikia kwamba ‘hakuna kazi rahisi duniani’, na kila jambo linalofanyika kwa kusudi fulani hugharimu nafasi ya binadamu. Kwa kuwa mtenda kazi hulipwa ujira wake, basi na taaluma yake ijengewe kingo za kumwongoza kuthamini huduma anayoitoa. image

image

Siku zote matokeo ya ubora wa kazi yoyote hutegemea kiasi cha hamasa na ari iliyotumika kufanikisha kazi husika, licha ya kwamba mahitaji au zana za kazi pia huchangia aina ya matokeo yanayozalishwa.
Ni kweli kuwa Serikali ndiyo msimamizi wa shughuli muhimu za umma katika jamii, na kutokana na uhaba wa rasilimali kulingana na mahitaji, imeeleza kuwa hujikuna kufikia mahali mkono unapoishia
Hili linaweza kuwa jawabu sahihi, lakini kwa dhamira na mpango madhubuti, yote yanawezekana kwa kuwa kilichosababisha iwepo haja ya kuwa na huduma ya kipolisi, kilisababisha pia haja ya kuwa na utumishi wa kitabibu (madaktari) na kujenga taaluma (waalimu).
Pamoja na kwamba zipo pia huduma nyingine ndani ya jamii ambazo nazo sharti zitazamwe na kupewa msukumo wa hamasa, lakini kama sera ni kujikuna mpaka mkono unapofikia, basi mpango mkakati wa awamu ndio utakaofanikisha haja ya kuondokana na umaskini kwa kujikomboa kutoka nyanja moja hadi yingine kwa nyakati tofauti.
Ni kwa nini kwanza iwe Polisi, madaktari na waalimu? Kwa mtazamo wa mapema unaweza kugundua kuwa ndizo shughuli zilizosheheni wafanyakazi wengi kupita maeneo mengine, lakini katika mfumo wa maisha tuliyonayo, nyanja hizi ndizo zinazotoa huduma zaidi kwa jamii na ndipo wengi wa wanajamii wanapogusa katika mahitaji ya kila siku.
Hivi karibuni Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Saidi Mwema, alizindua maduka maalumu ya watumishi wa Jeshi la Polisi mjini Moshi, maduka ambayo yatawaruhusu kupata huduma ya bidhaa mbalimbali ambazo zimeondolewa ushuru wa kodi.
Hili ni kundi la pili katika makundi makubwa yanayotoa huduma kwa jamii kufutiwa kodi, baada ya Jeshi la Wananchi nao kuwa na fursa hiyo kwa kipindi cha muda mrefu sasa.
Lengo la kuwaondolea watumishi hawa kodi kwa mujibu wa Inspekta Mwema, ni kuwaondolea ugumu wa gharama za maisha na kuwapa hamasa zaidi ya kutenda kazi kwa maslahi ya umma na kuepusha vishawishi vya rushwa.
Suala hili likitazamwa kwa undani zaidi, utakuta kwamba ugumu wa mazingira ya utendaji wa askari katika jamii yetu, unalandana pia na ule unaomkumba mwalimu na mhudumu wa afya.
Kimsingi, mkakati unapaswa kupangwa kuziwezesha jamii hizi kunufaika kutokana na kazi wanazozifanya, lengo likiwa kuhamasisha utumishi uliotukuka katika jamii.
Utumishi bora katika nyanja hizi unapoweza kukamilika, ni rahisi kugeukia nyanja nyingine na kama mkakati huu utaendelea, tukajikuta tumerahisisha maisha ya wananchi na kuondoa ugumu wa maisha katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

 
image
image
This text will be replaced
image