Polisi watimua wachimba kokoto Kunduchi
POlisi wakilinda machimbo yaliyosimasihwa kuchimbwa katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam leo, kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq. PICHA: ROMI 

Kikosi maalumu cha Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, leo kimewasili na kufanya operesheni katika eneo la machimbo ya kokoto katika ukanda wa Kunduchi, kuwaondoa wachimbaji wote eneo hilo, kufuatia amri ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Mhe Sadiq, wachimbaji hao walikatazwa kuendelea na kazi hiyo katika eneo hilo, kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa kutokana na uchimbaji huo.
Mkuu wa mkoa ameamuru polisi wa Kinondoni kukamatwa mara moja kwa wale wote wanaokaidi amri hiyo.
Aidha ameongeza kwamba uchimbaji wa mchanga na kokoto kwenye eneo hilo hususani pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo unaofanya na wachimbaji wadogo wadogo na wakubwa, unapaswa kusimama, kwa sababu unatishia usalama wa barabara hiyo kuu, pamoja na suala zima la mazingira kwenye eneo hilo.
Top Stories »





