News / Entertainment / Prof Jay alipuka, ni albamu ya ‘JAYSCO DAGAMA’

image

Prof Jay alipuka, ni albamu ya ‘JAYSCO DAGAMA’

By Editor

Profesa Jay akiwa katika pozi la ufukweni pamoja na baadhi ya vimwana (models) waliotumika katika shooting yake ya kibao cha ‘Kamili Gado’ kwenye fukwe za Kunduchi Beach Hotel Alhamisi ya wiki iliyopita. Picha: dar411 image

image

Vuta nikuvute ya muziki wa bongo nchini imeingia katika sura mpya baada ya mkongwe wa burudani ya muziki wa kizazi kipya Joseph Haule maarufu kama Jay wa Mutulinga ama Profesa Jay, kuibuka na kibao kipya cha video cha ‘Kamili Gado’ katika albamu yake mpya yenye jina JAYSCO DAGAMA.

Akizungumza na Dar411 katika ofisi za mtandao huo zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Prof Jay amesema alikamilisha shooting ya video hiyo siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita (09.02.2012), na kwamba itatolewa rasmi wiki ijayo.
“shooting ilikamilika alhamisi iliyopita na itakuwa released next week (itatoka wiki ijayo)” ametanabaisha Jay huku akisasambua baadhi ya mistari ya video hiyo.

Kibao hicho kilichorekodiwa na studio za MJ Records, akishirikishwa msanii Marco Chali, shooting yake (upigaji picha) ulifanyika kwenye fukwe za Hoteli ya Kunduchi (Kunduchi Hotel).

Kinachovutia katika muziki huu mpya wa Jay, ni jinsi alivyowatumia warembo halisia ambao wameelezwa kuwa hawajatumika katika video nyingine zozote zilizopita, na kwa mujibu wa Jay vimwana hao wametokana na mchanganyiko mbalimbali kutoka hapa nyumbani na nje ya nchi.

“Tulizunguka nyumba kwa nyumba mitaani kuwatafuta warembo hawa halisia” amesema Jay na kuongeza kuwa “lengo lake ni kwamba tunapoongea kuhusu ‘Kamili Gado’ tunataka ieleweke kwamba demu anawakilisha uhalisia wa mrembo kamili (aliyekamilika).”

Hali kadhalika mwanamuziki huyo mwenye umaarufu mkubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla, amebainisha kwamba warembo hao wapatao 17 hivi, wamepambwa na mbunifu maarufu nchini Mustafa Hassanali katika nkshi za hali ya juu, kwa ubunifu wa kipekee.

Pia pamoja na washiriki hao wa hapa nyumbani, kuna mchanganyiko wa wanadada wapatao wanne (4) kutoka nje ya nchi wakisherehesha na kuleta mvuto wa mchanganyiko katika upigaji huo wa picha (shooting).
Kwa picha za utayarishaji wa video hiyo, bofya hapa. Kwa maelezo zaidi kuhusu tukio hili jipya kwa maana ya siku na wapi kibao hiki kitakapozinduliwa na nyota huyo wa Bongo, kaa karibu na mtandao wako ‘www.dar411.com’ kupata vyote na vingine usivyovifahamu bado.

 
image
image
This text will be replaced
image