News / Sports / Simba, Azam dimbani leo Ligi kuu

image

Simba, Azam dimbani leo Ligi kuu

By dar411

Baada ya ngwe ya pili ya pazia la Ligi kuu Tanzania Bara kufunguliwa, Simba wanaingia tena kwenye kibarua kingine watakapoivaa timu ya Coastal Union kutoka Tanga kwenye dimba la Taifa, wakati katika uwanja wa Chamazi wenyeji wa uwanja huo Azam FC wataumana na African Lyon. image

image

Simba ambao walitolewa mapema katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni visiwani Zanzibar, imekuwa ikikosolewa kwa kukosa kiwango cha juu walipolazimika kuwaacha matajiri wa jiji Azam FC kutamba kwa kuwafunga na kisha kulitwaa kombe hilo.
Wekundu hao wa Msimbazi wanaingia dimbani kupambana na Wagosi wa kaya kutoka Tanga Coastal Union ambao nao wanasaka ushindi kwa hali na mali kujiweka katika nafasi njema katika msimamo wa ligi hiyo.
Wakati huo huo Chamazi Mbagala kunawaka moto wakati mabingwa wapya wa kombe la Mapinduzi Wanalambalamba Azam FC wanakutanishwa na watoto wa mjini African Lyon kwenye muendelezo wa Ligi kuu.

 
image
image
This text will be replaced
image