Tanzania na mfumko wa bei, kusitishwa kwa misaada na ufisadi
Wakati wananchi walio wengi wakiwa taabani kwa hali mbaya ya kiuchumi, ufisadi unaendelea kuzuru na kutafuna nyanja mbalimbali za maendeleo nchini, katika wakati ambao imesikitishwa kuona wahisani wamejiondoa katika mbio za kuokoa jahazi wakati huu mgumu. 

“siku ya kufa nyani miti yote huteleza” na Tanzania iko kwenye msukosuko (crisis) si tu wa kiuchumi bali pia wa kijamii kutokana na majeraha ya uchumi yanayoonekana kukosa tiba huku hatua mahususi kunusuru hali ya mambo zikienda mrema.
Wakati wananchi walio wengi wakiwa taabani kwa hali mbaya ya kiuchumi, ufisadi unaendelea kuzuru na kutafuna nyanja mbalimbali za maendeleo nchini, katika wakati ambao imesikitishwa kuona wahisani wamejiondoa katika mbio za kuokoa jahazi wakati huu mgumu.
Migogoro ya mafuta, hitaji kubwa la ajira, upungufu wa chakula, sakata la mgao wa nishati ya umeme, kuporomoka kwa thamani ya fedha ya ndani na bidhaa kupanda bei kila kukicha ni baadhi tu ya yale yaliyojisokota kwenye shingo ya Mtanzania.
Uamuzi wa Serikali za nchi Wahisani kutangaza kutoridhishwa na mwenendo wa Serikali wa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha, kumepelekea kiasi kikubwa cha mchango wa nchi hizo kusaidia bajeti ya Serikali kusitishwa na hadi sasa ni kiasi cha 7% pekee kitakachotolewa kwa Serikali.
Lawama kubwa katika hili zilielekezwa katika hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahujumu wakubwa uchumi (mafisadi) pamoja na usimamizi mbovu wa matumizi ya fedha za umma katika Halmashauri za vijiji na Manispaa.
Kwa hili, Maofisa wengi wa Serikali wamekuwa wakitapanya fedha zinazoelekezwa kwao kwa shughuli zisizokidhi haja ya lengo la kuwezesha na kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.
Aidha, sakata la mfumko wa bei halionyeshi mwisho wake, na uwezo wa Serikali na watu binafsi kukabili tatizo hili zinapungua.
Lakini hivi karibuni Serikali ilitangaza kuongeza fursa na matangazo ya nyanja za uwekezaji, ili kuondoa ile hali ya utegemezi kwa Wahisani katika bajeti ya Taifa.
Lakini ni kwa jinsi gani hatua hiyo inaweza kuokoa hali iliyopo sasa? Jibu ni kwamba huo ni mpango unaoweza kuleta mafanikio kwa miaka ya mbele iwapo utatekelezwa vyema kwa maslahi ya Taifa, lakini siku za hivi karibuni
Kuna maswali mengi katika hatua hiyo kutokana na historia ya masuala ya uwekezaji kunufaisha zaidi upande wa wageni kuliko wananchi.
Je, kwa mtindo huu, gharama za maisha zitapungua vipi? Kuna uwezekano wa mfumko wa bei kushuka na bidhaa kurudi masokoni kwa bei zinazowafaa wananchi? na je, inawezekana mikakati ya miradi ya maendeleo kuendelea kusonga mbele?
Ni changamoto nzito zinazofaa kufikiriwa kwa makini kuweza kujinasua na wimbi hili, kwa kuzingatia kwamba wakati tunapojiandaa kuchukua hatua, misaada ya kigeni imesitishwa huku
.
Top Stories »





