News /

image

TARCAIDS wataka ukimwi ukabiliwe kwa vitendo

By Editor

Mratibu wa Shirika la TACAIDS Badru Abdunuru akitoa mada kuhusiana na janga la Ukimwi kwa wadau mbalimbali wa Wilaya za Kigoma, Kasulu na Kibondo katika Ukumbi wa Ndela Mkoani Kigoma.
PICHA: ROMI
image

image

Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia masuala ya virusi vya ukimwi na maambukizi TARCAIDS, limewataka viongozi na wadau mbalimbali wa mkoa wa Kigoma kujitokeza katika kukabili janga la ukimwi kwa vitendo, kwa kuunda mikakati na kuishirikisha jamii kwa ukamilifu katika hatua za kuchukua.


Akizungumza na wadau mbalimbali kutoka mkoani hapo Mratibu wa shirika hilo Badru Abdunuru amewataka wadau hao kufanya vikao
vya mara kwa mara katika kupambana dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa
Ukimwi.

Katika kikao hicho cha siku moja kililchofanyika mwanzoni mwa wiki katika
ukumbi wa Ndela Mkoani Kigoma Abdunuru alisema, “kikao hiki kimewashirikisha
wadau kutoka katika Halmashauri za wilaya za Kigoma, Kasulu na Kibondo
ambao ni wawakilishi kutoka Shirika la Karitas, Concern, Jeshi la
wananchi wa Tanzania, Magereza, Polisi, Uhamiaji, Kividea, NWB,
Mtandao wa Cacon, Kikingonet, Kiungonet na Waratibu kutoka katika
Halmashauri za Wilaya”.

 
image
image
This text will be replaced
image