News / Sports / Timu ya Bunge kukipiga na Twiga Stars

image

Timu ya Bunge kukipiga na Twiga Stars

By dar411

Wabunge wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanatarajiwa kujitupa dimbani hapo Alhamisi wiki hii kusakata kabumbu dhidi timu ya Taifa ya soka ya Wanawake Twiga Stars, kabla ya kuwakabidhi zawadi zao. image

image

Akibainisha taarifa hiyo kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, msemaji wa shirikisho la Kandanda nchini TFF Boniface Wambura, ameeleza kuwa lengo la wabunge hao kucheza na Stars ni kuwapa hamasa katika mendeleo yao ya soka, na pia kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwwapa zawadi.
Ameongeza kuwa vijana hao wa Stars watakabidhiwa zawadi maalumu iliyoandaliwa na Bunge kwa ajili yao, wakati wakiwa katika harakati za mchezo wao wa mwisho wa marudiano na Namibia.
Itakumbukwa Stars katika kusaka nafasi ya kushiriki katika michuano ya Mataifa ya Afrika, ilifanikiwa kuitwanga timu ya Taifa ya Namibia kwa bao 2 bila majibu wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, na sasa wanatarajiwa kushuka tena dimbani Jumapili ijayo Januari 29 mwaka huu kurudiana nao katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


 
image
image
This text will be replaced
image