News / Sports / Twiga 2 Wabunge 1, wanyakua mil 10

image

Twiga 2 Wabunge 1, wanyakua mil 10

By dar411

Kikosi cha timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake Tanzania Twiga Stars, kimeibuka kidedea katika mchezo wake dhidi ya timu ya Muungano wa Wabunge, ambapo walifanikiwa kuwatungua kwa bao 2 kwa 1, na kisha kuzawadiwa Tsh milioni 10 zilizotokana na michango ya Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri. image

image

Mchezo huo uliopigwa hapo jana majira ya jioni kwenye dimba la Karume jijini Dar es Salaam, ulishuhudia Stars ikisakata soka la kuvutia, huku msisimko ukiwajaa zaidi mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano huo kwa kuwaona wabunge wakicheza kandanda.
Timu ya Wabunge mbayo iliundwa kutokana na uteuzi wa wabunge waliokuwa na uwezo wa kusakata gozi hilo, ilionyesha uhai kwa kuweza kumiliki pia mpira na kupiga pasi, suala ambalo halikudhaniwa na watazamaji wengi waliohudhuria.
Aidha baada ya mchezo huo kumalizika, kikosi hicho kinachonolewana Boniface Charles Mkwasa kilikabidhiwa zawadi ya fedha hizo milioni 10, kuwasaidia katika mchezo wao wa marudiano.
Stars itashuka dimbani Jumapili ijayo Januari 29, kupambana na timu ya Taifa ya Namibia katika ngwe ya pili na ya mwisho kusaka nafasi ya kutinga kombe la Mataifa ya Afrika. Itakumbukwa mchezo wa awali huko Namibia Stars ilishinda kwa bao 2 bila majibu.

 
image
image
This text will be replaced
image