Twiga Stars dimbani leo na Wabunge leo
Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake kwa mpira wa miguu Twiga Stars, kimejitupa uwanjani katika dimba la Karume, kuwavaa Waheshimiwa Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hatua ya kujifua kwa mchezo wa mwishoni mwa wiki. 

Mchezo huo uliotajwa na Wabunge hao kama hatua ya kuwapongeza kwa ushindi, kuwatia hamasa pamoja na kuwazawadia, unawahusisha wanawake wa bunge hususani wale vijana.
Kikosi cha Twiga Stars kimeibu shauku kubwa miongoni mwa wapenzi wa michezo nchini, baada ya kuleta matokeo mazuri kisoka, hususani wanaposhiriki katika michuano ya Kimataifa.
Timu hiyo inatarajiwa kupambana kwa marudiano na timu ya Taifa ya Namibia hapa jijini Dar es Salaam, katika mchezo huo utakafanyika kwenye uwanja wa Taifa baada ya kushinda katika mchezo wa kwanza wa nchini kwao kwa bao 2 bila majibu.
Top Stories »





