News / Sports / “Twiga Stars” shujaa asiyedhaniwa na wengi

image

“Twiga Stars” shujaa asiyedhaniwa na wengi

By dar411

Kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars, kimerejea jijini Dar es Salaam leo asubuhi kikitokea nchini Namibia ambapo walikwenda kupambana na timu ya Taifa ya nchi hiyo kutafuta nafasi ya kushiriki katika kombe la Mataifa ya Afrika huko Equatorial Guinea Novemba mwaka huu. image

image

Wakiwa na furaha, wachezaji wa timu hiyo waliamsha hisia za shangwe na hoihoi kwa mashababiki wachache waliokwenda kuipokea timu hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere alfajiri ya leo, baada ya kufanikiwa kuwashinda Wanamibia kwa bao 2 bila majibu.
Ikisakata kandanda safi huku wakielewana vilivyo dimbani, Twiga ilijipatia mabao yake katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa nyota wake Asha Rashid na Mwanahamisi Shaluwa na kuwahakikishia ushindi.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Sam Nujoma jijini Windhoek Namibia Ijumaa mwishoni mwa Juma, uliwaweka Stars katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, ambapo watarudiana na Wanamibia hao nyumbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwezi huu tarehe 29.
Iwapo kikosi hicho kitathibitisha ushindi wake katika mchezo huo wa marudiano jijini Dar es Salaam, huenda kikosi hicho kikawakwaa warembo kutoka Misri, watakaokutana nao katika hatua inayofuata.
Timu hiyo ya wanawake Twiga Stars imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali hasa ya Kimataifa, licha ya kukumbwa na adha ya kukosa fedha na mahitaji mbalimbali, ambapo wafadhili na wadhamini wengi wamekuwa wakielekeza nguvu kwenye timu ya soka ya wanaume Taifa Stars na kuisahau timu hiyo inayopeperusha vyem zaidi bendera ya Taifa Kimataifa ukilinganisha na wanaume.

 
image
image
This text will be replaced
image