Twiga Stars kambini kumaliza kazi
Baada ya kurudi na ushindi wa bao 2 kwa nunge kutoka Namibia, kikosi cha timu ya soka ya Wanawake Twiga Stars kimeanza mazoezi tayari kwa mchuano wa pili wa marudiano na wapinzani wao kutoka Namibia utakaofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi. 

Twiga ambao wanaongozwa na kocha Charles Boniface Mkwasa wameingia kambini katika hali ya furaha, wakiarajia kuthibitisha ubora wao watakapowakaribisha Namibia katika uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wao.
Licha ya kuwa katika matatizo lukuki ya kifedha, kikosi hicho kimekuwa kikifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali hususani ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa shirikisho la kandanda nchini Angetile Hoseah hapo jana, TFF inawakaribisha na kuwahamasisha wananchi mbalimbali walioguswa na timu hiyo pamoja pia na makampuni mbalimbali kujitokeza kuichangia timu hiyo iweze kujimudu kisoka.
Top Stories »





