U-turn, Vodacom watoa mil 10 kwa yatima
Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Vodacopm, Mwamvita Makamba, wakifurahia pamoja na watoto yatima jijini Dar es Salaam leo.
PICHA:ROMI


Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu Kurasini jijini Dar es Salaam, leo kimepokea misaada ya vyakula na mahitaji mengine yote yakiwa na thamani ya Tsh milioni 10, kutoka kwa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom pamoja na mtandao wa U-turn.
Wakiwa pamoja, mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa mahusiano, masoko wa Vodacom Mwamvita Makamba, wamefanya tafrija kuburudika na watoto hao, katika kuwafariji na kuwaonyesha umoja ulio sawa na watoto wengine.
Kituo cha watoto yatima Kurasini jijini Dar es Salaam, ni moja tu ya vituo vya watoto hao wenye uhitaji wa misaada ya kijamii, ambapo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa na wanaharakati na watu binafsi pia Serikali katika kuihamasisha jamii kujitolea kwenye kuyasaidia makundi haya ya wahitaji kuweza kumudi gharama za maisha.
Top Stories »





