News / Entertainment / Valentine Day, wahanga wa fistula wachangiwa

image

Valentine Day, wahanga wa fistula wachangiwa

By Editor

Wafanyakazi na watendaji wa Kampuni ya simu za mikononi Vodacom Tanzania, wakiwa katika hafla ya Sherehe za siku ya Wapendanao duniani leo, zilizofanyika katika ofisi zao mpya zilizoko eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam,wakilenga kuchangia fedha kusaidia matibabu ya fistula kwa wakina mama. PICHA: ROMI image

image

Katika kusheherekea sikukuu ya wapendanao duniani ‘Valentine Day’ inayoadhimishwa siku kama ya leo (14.02.) kila mwaka, wafanyakazi na watendaji wa kampuni ya simu za mikononi Vodacom, wamejitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula kupitia kampeni yao ya MOYO.

Sherehe hizo zilizofanyika leo katika ofisi mpya za kampuni hiyo kwenye eneo la Mlimani City Dar es Salaam, ziliongozwa na Mkurugenzi wake Mtendaji Rene Meza na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwanvita Makamba.

Wakiwa katika hali ya furaha na shangwe huku wakicheza muziki, wafanyakazi hao wameendelea na kazi ya kuchangia fedha katika mfuko huo maalumu wa ‘MOYO’, ulioratibiwa na kuendeshwa na kampuni hiyo kusaidia matibabu ya matatizo a fistula kwa wanawake.

Kilele cha kampeni yao hiyo ya kuchangia fedha kwa matibabu ya Fistula
kitahitimishwa kwa hafla maalum itakayohudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete
kama mgeni rasmi mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

 
image
image
This text will be replaced
image