News / Entertainment / Vazi rasmi la Taifa, sasa wananchi kuamua

image

Vazi rasmi la Taifa, sasa wananchi kuamua

By dar411

Baada ya Wabunifu mbalimbali kutoa mapendekezo yao juu ya aina ya vazi rasmi la Kitanzania, mchakato huo sasa umeelezwa kupelekwa kwa wananchi, kwa ajili ya kupata maoni yao kupitia kwa kamati maalumu iliyoundwa. image

image

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, mchakato huo unaendelea vyema, na kwamba hatua za awali za zoezi hilo za kupata mapendekezo ya vazi stahiki zimeshatekelezwa kupitia wabunifu wa ndani.
Aidha mchakato huo umeelezwa kupata taarifa za kiuzoefu kutoka Mataifa ya Kiafrika ambayo tayari yameshapitia hatua kama hiyo, wakiwemo Ghana, Swaziland, Ethiopia na Mali.
Miongoni mwa wadau waliotajwa kuunda Kamati itakayoshughulikia suala la utafutaji wa maoni ya wananchi ni pamoja na Mwenyekiti Joseph Kusaga, akisaidiwa na Angela Ngoyi, Joyce Mhavile, Habib Gumze na Hasanali Mustafa miongoni mwa wengine.
Kamati hiyo iliyoteuliwa na Waziri wa Habari Mhe Emmanuel Nchimbi, imetakiwa kuanza kazi yake rasmi kuanzia siku tatu zijazo.
Mapema mwaka 2004, Serikali ilichukua uamuzi wa kuratibu upatikanaji wa vazi rasmi la Taifa, katika mchakato ambao ulianzia kwenye hatua ya ubunifu ulioendeshwa kupitia wanamitindo tofauti nchini, hadi kufikia wakati huu ambapo baada ya udunifu kufanyika, sasa ni kutafuta maoni ya wananchi.

 
image
image
This text will be replaced
image