Wageni wataka biashara ya madafu itangazwe
Baadhi ya raia wa nchi za nje wakifurahia madafu katika ufukwe kandakando ya barabara ya Ocean jijini Dar es salaam leo. PICHA:ROMI


Baadhi ya wageni waliokuja nchini wamebainisha kufurahishwa kwao na bidhaa ya madafu yanayotokana na zao la mnazi, kwa kueleza kwamba ni bidhaa inayoweza kuwa na wateja wa kutosha na kuipatia nchi kipato.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika eneo la Ocean Road jijini Dar es Salaam leo, wageni kutoka Mataifa mbalimbali duniani wameonyesha furaha yao kwenye bidhaa hiyo inayosambazwa kwa wingi jijini Dar es salaam, wakisema inaburudisha.
Raia hao ni baadhi ya washiriki wa mkutano wa kimataifa wa watoto
unaofanyika jijini, ambao umeandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la ‘Save the Children’ ambalo linajihusisha na maslahi ya
watoto hapa nchini.
Top Stories »





