News / Business / Stakabadhi ghalani sasa kwenye mpunga

image

Stakabadhi ghalani sasa kwenye mpunga

By dar411

Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilali, amewataka wakulima wa mpunga na mazao mengine mkoani Tanga, kujiunga na mfumo wa Stakabadhi ghalani, ili kuwapeusha na ulanguzi unaofanywa na wanunuzi wa mazao yao. image

image

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Scheme ya umwagiliaji ya zao la Mpunga Mombo wilayani Korogwe Tanga, Dr Bilali amesema ni vyema wakulima hao wakajiunga na mfumo huo, ili kuwalinda kutokana na udanganyifu unaofanywa na walanguzi.
Scheme hiyo ambayo pia inatarajiwa kuwa na kiwanda chake cha usindikaji, imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na uzalishaji wenye tija.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Meneja uzalishaji wa Scheme hiyo Samson Mwembe amesema kiwanda hicho kinalenga kuimarisha zaidi uzalishaji huo kwa kuweza kuuza mchele badala ya kuuza mpunga kama ilivyo sasa.
Itakumbukwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani ulianzishwa miaka michache iliyopita kwa wakulima wa zao la Korosho kwenye mikoa ya Pwani kujiunga na mfumo huo, ulioonekana kuwa na matunda kutokana na wakulima hao kuweza kuuza mazao yao yote na kuepuka kupata hasara ya kuharibika kwa kukosa soko, huku pia wakihakikishiwa usalama wa fedha zao, japo wanazipata kwa awamu.

 
image
image
This text will be replaced
image