News / Business / Mgogoro wa wakulima, wanyamapori wazidi

image

Mgogoro wa wakulima, wanyamapori wazidi

By Editor

Afisa wa Wanyamapori John Makotta akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa (kushoto) wakati Waziri huyo alipotembelea Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro. PICHA: ROMI
image

image

Katika ziara yake kwenye bonde la mto Kilombero mkoani Morogoro, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Dkt Terezya Huviza amesema mgogoro unaoghubika eneo la mpaka baina ya wakulima wa eneo la Kilombero dhidi ya Idara ya Wanyama pori unapaswa kumalizika mara moja ili kuepusha kuzorota kwa uchumi kwenye eneo husika.

Akizungumza na Afisa wa Wanyamapori katika eneo lenye mgogoro John Makota, Waziri Huviza ametahadharisha kwamba pande husika zinaweza kukabiliana na mdororo wa kiuchumi iwapo masuala ya mgongano yataendelea kuwakabili.

Wakulima wa mpunga katika wilaya ya Ulanga wamekuwa wakilaumiwa na Idara ya Wanyamapori katika eneo hilo kwa kuvuka mpaka na kuingia kwenye maeneo tengefu ya hifadhi ya Wanyamapori.
Idara hiyo inawalaumu wakulima hao kwa kuwa wanasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye maeneo husika, katika wakati ambao wakulima nao wanailaumu idara hiyo kuwa inawabughudhi katika shughuli zao za kilimo.

 
image
image
This text will be replaced
image