News / Local News / Wizara yagomewa, madaktari watoweka vituoni

image

Wizara yagomewa, madaktari watoweka vituoni

By dar411

Tamko la Serikali hapo jana kuwataka madaktari kuendelea na madai yao wakiwa vituoni limekuwa kama sumu kwa madaktari hao, ambapo Hospitali nyingi zimeripoti kutoonekana kabisa kwa matabibu hao, na hata Manesi waliokuwa wakionekana jana nao wametoweka. image

image

“Mi nlichoomba jana ni warejee kazini, halafu bado forum ipo wazi, lakini wenzetu hawaji!” ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Haji Mponda akizungumzia sakata hilo leo asubuhi, ambapo amethibitisha kuwa Hakuna daktari aliyekwenda kwake kwa mazungumzo na kwamba mgomo umeendelea.
Dr Mponda amekiri kuwa mgomo huu ni mgogoro wa aina yake, na kufafanua kuwa baadhi ya madaktari wanahudhuria vizuri hospitalini kusaini na baada ya muda wanakwenda kusikojulikana.
Taarifa kutoka katika vituo mbalimbali vya tiba nchini hususani hospitali kubwa za mikoa, imesema hali ya wagonjwa imezidi kuwa tete na mazingira ya hospitali hizo kupata kimya cha ajabu, kutokana na kutoonekana hata wauguzi wadogowadogo waliokuwa wakizungukazunguka vituoni humo jana.
Katika Hospitali ya Taifa ya Morogoro na Dodoma wodi zimeonekana zikiwa na wagonjwa tu bila wahudumu, huku pilikapilika za Manesi zikipungua kwa kutoonekana kwa wengi wao.
Wakati huo huo baadhi ya Hospitali zimefanikiwa kuendesha huduma za dharura pekee, ambapo madaktari bingwa wamejikita katika zoezi la huduma hizo za dharura, na kwamba zile za kawaida hazishughulikiwi kutokana na wingi wa wagonjwa waliofurika vituoni.

 
image
image
This text will be replaced
image