Kibarua cha Yanga sasa kuhamia Misri
Mabingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam, ilishindwa kujipatia ushindi dhidi ya wapinzani wake wa Kiarabu kutoka Misri Zamalek,licha ya kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, na sasa imebashiriwa kukumbwa na kibarua kizito Misri licha ya kwamnba mashabiki wa Misri hawataingia uwanjani. 

Yanga ambayo ilijipatia goli la kuongoza katika dakika za awali, ilishindwa kujiongezea mabao zaidi na kujikuta ikikosa nafasi za wazi,hali huku walinzi wake wakisababisha makosa yaliyopelekea goli hilo kusawazishwa dakika za mwisho na mshambuliaji mahiri wa Zamalek Amri Zakky.
Kutokana na sare hiyo, mabingwa Yanga watalazimika kushinda ugenini Misri wakati watakapokutana na Waarabu hao katika mchezo wa marudiano.
Itakumbukwa kuwa watacheza bila mashabiki kutokana na shirikisho la soka Misri kupiga marufuku mashabiki kuhudhuria uwanjani kutokana na vifo vya watazamanji zaidi ya 70 pamoja na askari wa usalama waliokufa kutokana na vurugu kwenye mchezo wa Ligi kuu ya huko baina ya mahasimu Al Ahly dhidi ya Al Masri siku chache zilizopita.
Top Stories »





