Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, kimerejea nchini hii leo kikitokea Ivory Coast kilikokuwa kikishiriki mchezo wa maandalizi ya kucheza fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri chini ya miaka 20.
Akizungumza baada ya kurejea, kocha msaidizi wa kikosi hicho Adolf Rishard amesema makosa madogomadogo ya vijana wake pamoja na kuwakosa baadhi ya wachezaji ndicho kisa kuupoteza mchezo wao na Ivory Coast na kwamba sasa wanajipanga upya.
Mchezo huo ambao Stars ilikuwa ikicheza ugenini, ilijikuta ikifungwa bao 1 bila majibu. Kwa mujibu wa kocha huyo, timu hiyo ina wakati mgumu wa kuhakikisha inashinda kwa kiwango kizuri mchezo ujao wa marudiano ambapo vijana wa Tanzania watapata usaidizi wa kutosha kutoka kwa mashabiki wake.
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: