Home |
Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather |
|
Entertainment
In this section you can find out the latest news and gossip in Bongo, the hottest music videos from your favorite artists and from a few up and coming acts, what celebrities got up to while they were at school, the latest street words, and what's happening in your favorite soap opera. EntertainmentKinondoni wazindua rasmi mkakati wa usafi
Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni, imezindua rasmi mpango uliotangazwa mapema na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. William Lukuvi wa kuanzisha mfumo madhubuti wa kusafisha na kuhifadhi mazingira ya jiji.
![]() Akizindua mpango huo kwa Wilaya ya Kinondoni katika viwanja vya Biafra jana mchana, Mkuu wa Wilaya hiyo Geordon Lugimbana amebainisha kuwepo sheria katika Wilaya hiyo zitakazosaidia kuwatia hatiani na kuwaadhibu wachafuzi wa mazingira na hivyo kuhimiza utaratibu mpya wa ustaarabu uanze kujengwa miongoni mwa wakazi ili kulitunza jiji.
‘Sasa Kinondoni tuna sheria za usafi, na tunaweza kumkamata mtu kisha sheria zinatuongoza kwenye hatua za kuchukua’ amefafanua Lugimbana
Kadhalika Mhe. Lugimbana amewasifu wakuu wa idara kwa kutekeleza kwa mafanikio suala la kuhakikisha ujenzi wa madarasa na upelekaji wa watoto wote mashuleni mwaka jana na kuwataka sasa kuhamishia juhudi hizo kwenye suala la usafi kuanzia mwaka huu. Pia mkuu huyo wa Wilaya amewaka wenyeviti wote wa Serikali za mitaa kuwasilisha kwake kila mmoja mpango wake wa mkakati wa usafi, kutenga eneo maalumu la kulundika taka mtaani kwake, kuunda mpango thabiti na wa uwazi wa kukusanya ada ya usafi kutoka kwa wakazi pamoja na kuajiri vijana wasiopungua 20 kwa ajili ya kukusanya taka kutoka majumbani na kupeleka kwenye dampo la mtaa. ReviewsComment Preview More on EntertainmentLive Music
This text will be replaced by the flash music player.
![]() |
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: