Tuhuma zilizokuwa zinalikabili kampuni moja la Mafuta nchini juu ya kuliuzia shirika la reli nchini TRL mafuta yaliyosadikika kuwa yamechakachuliwa, zimepingwa baada ya tafiti za taasisi mbalimbali kuonyesha kuwa mafuta hayo ya Diesel ni salama kwa matumizi.
Kwa mujibu wa Afisa uhusiano wa TRL Midrad Mayezi tume iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi imetoa ripoti yake tarehe 22 mwezi huu kisha nao EWURA wakafanya utafiti wao wa kiwango cha kimataifa SGS na kugundua kuwa mafuta hayo hayakuwa na mchanganyiko wowote.
Mafuta hayo yaliyopelekwa katika Shirika hilo kwa ajili ya kuendeshea mashine za treni yamekuwa katika hifadhi kusubiri ripoti za uchunguzi, baada ya sampo za mafuta hayo kuchukuliwa kwa uchunguzi.
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: