Kikosi cha timu ya Simba kilichopo katika maandalizi ya kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kimethibitisha kuwasili kambini leo kwa mshambuliaji wake wa kutumainiwa Musa Hssan Mgosi aliyekosa mazoezi ya awali ya timu hiyo.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji Mkuu wa timu hiyo Clifford Ndimbo amesema kwa sasa wachezaji waliosalia ambao bado hawajaripoti ni watatu tu, ambao ni Emmanuel Okwi, Joseph Owino na Patrick Ochwan.
Aidha katika hatua nyingine uongozi wa kamati kuu ya Klabu hiyo ya Simba unategemewa kukutana katika mkutano wa dharura kujadili suala la Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri ambaye bado hajawasili katika kikosi hicho, akiwa safarini nyumbani kwao Zambia.
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: