Home |
Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather |
|
Entertainment
In this section you can find out the latest news and gossip in Bongo, the hottest music videos from your favorite artists and from a few up and coming acts, what celebrities got up to while they were at school, the latest street words, and what's happening in your favorite soap opera. EntertainmentNizar, Nadir watamba Canada
Nadir Haroub 'Cannavaro' na Nizar Khalfan wachezaji wa Timu ya Taifa ambao waliondoka wiki iliyopita kwenda nchini Canada wamelivutia benchi la ufundi la timu ya Vancouver Whitecaps na wanaweza kusajiliwa kwa mkataba muda wowote.
Naibu Meneja wa Kampuni ya LZ Enterprises, Rahim Kangezi alisema ya kuwa wachezaji hao kesho watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Toronto FC na baada ya mechi hiyo watajua nini kinachoendelea.
Kangezi alisema kuwa
![]() Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Nizar Khalfan wachezaji wa Timu ya Taifa ambao waliondoka wiki iliyopita kwenda nchini Canada wamelivutia benchi la ufundi la timu ya Vancouver Whitecaps na wanaweza kusajiliwa kwa mkataba muda wowote. Naibu Meneja wa Kampuni ya LZ Enterprises, Rahim Kangezi alisema ya kuwa wachezaji hao kesho watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Toronto FC na baada ya mechi hiyo watajua nini kinachoendelea. Kangezi alisema kuwa Khalfan na Cannavaro wameonyesha uwezo mkubwa tangu walipowasili nchini humo Julai 3 na hakuna shaka kuwa watafanya vema siku za usoni na kuingia mkataba. Aliongeza kuwa, timu hiyo inataka kujiimarisha zaidi katika ligi hiyo na wachezaji hao wawili ni miongoni mwa tegemeo lake katika ligi. “Waliwaona siku ambayo timu hiyo ilipocheza na Yanga na Taifa Stars, wakaridhika na kiwango chao, vile vile, wameonyesha uwezo zaidi huko, bila shaka watafanikiwa na kuwa wachezaji wa kwanza kucheza soka ya kulipwa Amerika ya Kaskazini” alisema Kangezi. Alisema kuwa bado wanatarajia Zahoro Pazi kujiunga na wenzake muda wowote baada ya kukamilika kwa taratibu za kusafiri na za kiufundi. “Pazi anatakiwa kujiunga na wenzake ndani ya wiki mbili na tayari mipango hiyo ipo mbioni” alisema. Wakati huo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Boniface Ambani anaondoka leo jioni kwa ndege ya Emirates kwenda China kucheza soka ya kulipwa. Ambani alisema jana kuwa anaondoka leo, lakini bado hajawa na uhakika kama kweli atabaki huko au la kutokana na mambo fulani ambayo bado hawajafikia muafaka na timu hiyo. “Siwezi kusema kama naenda sitarudi tena, ila, nakwenda China nikiwa mguu ndani mguu nje na kama tukishindwa kufikia muafaka ndani ya wiki moja nitakuwa Dar es Salaam,” alisema. Alisema endapo atasajiliwa katika timu hiyo, itakuwa faraja kwake kwani malengo yake yatakuwa yametimia kwani awali kabla ya kutua Yanga alikuwa anacheza soka ya kulipwa nchini India. ReviewsComment Preview More on EntertainmentLive Music
This text will be replaced by the flash music player.
![]() |
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: