Home | Dar-es-Salaam weather Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather
RSS News
Entertainment

In this section you can find out the latest news
and gossip in Bongo, the hottest music videos from
your favorite artists and from a few up and coming acts,
what celebrities got up to while they were at school,
the latest street words, and what's happening in your
favorite soap opera.

Entertainment

Phiri atemwa rasmi Simba
Klabu kongwe ya soka nchini Simba Sports Club, imemtangaza rasmi kocha mpya wa kukinoa kikosi hicho kuchukua nafasi ya kocha Mzambia Patrick Phiri, aliyedaiwa kukiuka baadhi ya vipengele vya mkataba wake, ikiwemo kuchelewa kufika Klabuni kuiandaa timu.

Kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Klabu hiyo Evodius Mtawala, kikao cha kamati kuu ya Klabu hiyo kimeamua kumtangaza kocha raia wa Serbia Milovan Sikovic, na kumkabidhi kibarua chenye mkataba wa miaka miwili kuifundisha Simba.

Amesema kutokana na kazi nzuri pia ushirikiano mzuri aliouonyesha kocha wa zamani Phiri, wameamua kumtumia barua ya kumuomba aandike barua ya kusitisha mkataba wake, ili isionekane Simba wamemfuta kazi, kwa lengo la kulinda heshima yake katika soka.

‘Kikao cha kamati kuu kimemwomba aandike barua ya kuterminate mkataba wake, ili suala hilo lisipelekwe FIFA na kumuharibia CV yake,’ amesema Mtawala

Simba kwa sasa inajifua chini kocha msaidizi Sule Said Mziray huko Zanzibar katika mazozi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi, utakaotanguliwa na mechi ya ufunguzi ya ngao ya hisani dhidi ya wapinzani wake Yanga.

Reviews


Comment Preview

Name:

Email: 

Smileys

Remember my personal information
Notify me of follow-up comments?


Submit the word you see below:



Live Music

This text will be replaced by the flash music player.