Home | Dar-es-Salaam weather Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather
RSS News
Entertainment

In this section you can find out the latest news
and gossip in Bongo, the hottest music videos from
your favorite artists and from a few up and coming acts,
what celebrities got up to while they were at school,
the latest street words, and what's happening in your
favorite soap opera.

Entertainment

Silaha 5,000 zateketezwa Morogoro
Serikali mjini Morogoro imeteketeza kwa kuchoma moto silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki na bastola zilizokuwa zinamilikiwa na baadhi ya wakazi na makampuni bila kibali maalumu kinyume na sheria.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri, mkuu wa mkoa wa Morogoro Kanali Mstaafu Issa Machibya amesema silaha hizo haramu zimeleta madhara makubwa vikiwemo vifo vya baadhi ya raia, kusababisha majeraha na kutishia amani kwa ujumla kutokana na matukio ya kijambazi.

Nayo taarifa ya polisi imebainisha kuwa chanzo kikuu cha silaha zote hizo zilizokuwa zikimilikiwa kiholela ni kutokana na wimbi la wakimbizi wanaotoka katika nchi mbalimbali kama Burundi na Kongo, pamoja na ambazo zinaingia nchini kihalifu na kwa matukio ya kihalifu.

Aidha Jeshi la Polisi limeeleza mkakati wa kuzihakiki silaha zote zinazomilikiwa na watu binafsi pamoja na makampuni na kuzipiga alama maalumu silaha hizo, kuweza kuzitofautisha au kuzipa utambulisho maalumu.

Reviews


Comment Preview

Name:

Email: 

Smileys

Remember my personal information
Notify me of follow-up comments?


Submit the word you see below:



Live Music

This text will be replaced by the flash music player.