Home | Dar-es-Salaam weather Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather
RSS News
Entertainment

In this section you can find out the latest news
and gossip in Bongo, the hottest music videos from
your favorite artists and from a few up and coming acts,
what celebrities got up to while they were at school,
the latest street words, and what's happening in your
favorite soap opera.

Entertainment

TAKUKURU fanya kazi yako-Makamba
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM sawa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho Pius Msekwa, wameunga mkono hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, kuwakamata baadhi ya makada wao wa chama hicho kwa kutuhumiwa kuhusika na masuala ya rushwa.

Akizungumzia suala hilo jijini Dar es Salaam leo, Makamba amesema mwanachama wa chama hicho atakayethibitika kuhusika na suala la rushwa hatatetewa kwa kuwa ni kinyume na utaratibu na pia katiba ya chama inakataza.

‘kama mtu atashikwa, TAKUKURU endelea naye’ amefafanua Makamba

Naye Kaimu mwenyekiti wa Chama hicho Pius Msekwa amesema rushwa ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine kama ya wizi au mauaji, na kwamba sheria inapaswa kutenda inavyotakiwa.

Reviews


Comment Preview

Name:

Email: 

Smileys

Remember my personal information
Notify me of follow-up comments?


Submit the word you see below:



Live Music

This text will be replaced by the flash music player.