Home | Dar-es-Salaam weather Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather
RSS News
Entertainment

In this section you can find out the latest news
and gossip in Bongo, the hottest music videos from
your favorite artists and from a few up and coming acts,
what celebrities got up to while they were at school,
the latest street words, and what's happening in your
favorite soap opera.

Entertainment

Yanga yawanyuka Wakenya
Timu ya soka ya Yanga kutoka Dar es Salaam, imefanikiwa kuibuka kidedea katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Klabu ya soka kutoka Kenya AFC Leopard, baada ya kuwanyuka kwa bao 1 bila majibu katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid cha mjini Arusha yalipo makazi ya Klabu ya soka ya AFC ya mjini Arusha.

Akizungumza baada ya mchuano huo mkali baina ya vinara hao wawili, Kocha Mkuu wa Klabu ya AFC Leopard kutoka Kenya Dino Kitavi amesema timu ya Dar Young Africans imestahili ushindi kutokana na uzoefu wake kisoka, na kuongeza kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili.

Wakati huo huo kitendawili kimezidi kutawala juu ya uwanja gani Yanga itumie kwa michezo yake ya nyumbani, baada ya Serikali kusuasua kutoa majibu juu ya ombi lao la kuutaka uwanja wa Taifa , hivyo kulazimika pia kujiandaa kutumia kiwanja cha Jamhuri mjini Morogoro kama ombi hilo litatupiliwa mbali.
hata hivyo kwa taarifa hazijathibitishwa zilizotufikia hivi karibuni, zinasema tayari Wanajangwani hao Yanga wamesharuhusiwa kutumia kiwanja hicho cha Jamhuri mjini Morogoro.

Reviews


Comment Preview

Live Music

This text will be replaced by the flash music player.