Mabingwa watetezi wa Kombe la Vodacom Ligi kuu Tanzania Bara Yanga wameshusha kichapo cha mwaka na kuibua kilio kwa Wanaturiani Mtibwa Sugar wa mji kasoro bahari Morogoro, katika mchezo uliopigwa jioni ya leo.
Mabingwa hao wa Jangwani wamejipatia mabao matatu dhidi ya moja la Mtibwa licha ya wapinzani wao hao Mtibwa kumiliki vizuri mchezo huo kuwapita Yanga. Mtibwa wamepoteza nafasi nyingi za wazi lakini wapinzani wao wamezitumia zao vilivyo.
Yanga wako katika maandalizi ya michuano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Lupopo ya Congo itakayochezwa siku chache zijazo.
Mchezo mwingine wa Ligi kuu utapigwa hapo kesho ambapo vinara wa Ligi hii Wekundu wa Msimbazi Simba wataivaa Manyema FC katika mchezo ambao baadhi ya wachezaji wa Simba waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini huku wengine wakijiandaa kuanza mazoezi baada ya kupona majeraha.
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: