Home | Dar-es-Salaam weather Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather
RSS News
Entertainment - News
In this section you can find out the latest
news and gossip in Bongo, the hottest
music videos from your favorite artists and
from a few up and coming acts, what
celebrities got up to while they were at
school, the latest street words, and
what's happening in your favorite soap opera.
Fataki zapigwa marufuku sikukuu kesho
Wakati Jumuiya ya Kiislamu nchini ikijiandaa kwa sikukuu ya Eid El Fitri kesho Ijumaa baada ya mwezi kuandama jioni hii, shambrashambra za kusheherekea siku hiyo kwa kupiga fataki juu zimepigwa marufuku huku Jeshi la Polisi likitoa angalizo kwa suala zima la usalama.
Utata kiwanda cha Mtibwa Morogoro wazimwa
Sakata la malumbano na kutoelewana baina ya Wamiliki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha mkoani Morogoro, umepatiwa ufumbuzi baada ya kauli ya Raisi Kikwete iliyowataka wahusika kufanya mkutano wa kumaliza mvutano mara moja.
Uzalishaji wa sumu sasa kudhibitiwa Dar
Asasi mbalimbali za kuhifadhi mazingira kwa kushirikiana na Shirika la viwango nchini TBS, leo wamekubaliana kupitisha rasimu ya viwango vya mabaki yanayotakiwa kuingizwa katika mazingira, kwa lengo la kuepusha uchafuzi wa mazingira yetu.
Prof Jay: akana kukutana na Bill Gates
Hivi Karibuni zilitapakaa Habari kwenye mitandao ya Internet kuwa Msanii wa Hip Hop Prof Jay amekutana na tajiri mwenye mkwanja mrefu duniani Bill Gates katika ofisi zake na kuongea mawili matatu.
Alikiba Ajitoa Records
baada ya kufanya kazi na G Records, kwa Takribani miaka kadhaa tangu utambulisho katika industry ya Bongo Fleva msanii wa kizazi kipya Ali kiba ameamua kuachana na uongozi huo na kuamua kufanya kazi zake mwenyewe.
Godzilla: Kuzindua Godzilla Inc
Msanii wa bongo fleva anayejulikana kwa jina la Godzilla King of Salasala ameanzisha lebo yake inayokwenda kwa jina la Godzilla Inc! GodZilla amesema lebo hiyo itakuwa ikiwasupport wasanii undergrounds wanao chana lakini hawajapata nafasi ya kuingia studio
Ben Pol = Msanii anayekuja kwa kasi
Ni msanii anayekuja kwa kasi na ni mmoja wa vijana aliye chini ya usimamizi wa Duke Tachez kutoka M lab studio ambayo iko chini ya Duke. Jina lake Halisi ni Benard Paul mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne, lakini kwa jina la kisanii anajulikana zaidi kama Ben Pol. Ben Pol alianza kujigundua kuwa ana kipaji cha muziki akiwa Darasa la Tano ambapo nyimbo yake ya kwanza aliandikiwa na Baba yake mdogo hiyo ilikua mwaka 2001. na akaachana na mambo ya muziki na kufanya sanaa za shule zaidi ikiwa na kuigiza na mambo mengine.
Pingamizi la Kikwete, CHADEMA kutoenda Mahakamani
. Tendwa asisitiza uamuzi wake kufuta pingamizi hilo ni sahihi . Wananchi waaswa kupima uhalali wa maamuzi hayo ya tume Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini CHADEMA, kimejibu uamuzi wa Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kuwa si madhubuti haukutenda haki na haukuzingatia kiini halisi cha pingamizi lenyewe, na kusisitiza kuwa bado wanahitaji haki itendeke.
Ramadhani, Biashara ya abiria Ubungo yadoda
Wafanyabiashara ya usafirishaji wa abiria waendao mikoani katika kituo kikuu cha Mabasi Ubungo, wameeleza kukumbwa na wakati mgumu baada ya wateja wa biashara yao kupungua kutokana na sikukuu ya Ramadhani.
Makamba aipongeza CCM kwa ushindi wa pingamizi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Luteni mstaafu Yusuf Makamba, ametoa pongezi kwa uamuzi wa Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa, uliofuta pingamizi dhidi ya Mgombea wa CCM juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Page 1 of 82 pages  1 2 3 >  Last »