|
- Events in Pictures
Dar411 lets you share the fun and events
that occur daily in the streets. Do you miss
"hekaheka za kitaani kwenu", Mchiriku, or
anything else from your streets ? Here are
events in pictures that will bring you closer to
your street.

Parking nyingine jamani, hili ni gari la mradi mkubwa kabisa likiwa limepakiwa hapo, sijui wanamuogopa au ndiyo style mpya ya kupaki, tusaidie Mwananchi.

Kondakta wa daladala moja lifanyalo safari zake kati ya gongo la mboto - sinza akikwidana mashati na jamaa mmoja inaesadikika kuwa alikuwa ni abiria katika gari hilo baada kupishana kauli na jamaa huyo wakati akidai chake.

Hili shimo lililopandwa na mti mkavu, inasemekana lipo hapo kwa siku nyingi sana sasa lakini hakuna hata anaeshughulika nalo, lipo katika barabara ya msimbazi usoni kabisa mwa kituo cha Polisi Msimbazi.

Kweli Bongo Noma, Jamaa pamoja na kuwa ni njia ya Treni pale maeneo ya Buguruni lakini Biashara inaendelea kama kawaida...!

Kusema kweli utafutaji mwengine wa maisha ni hatari, hebu muangalie huyu Jamaa kama alivyokutwa mchana huu maeneo ya Ubungo akiiba mafuta kwenye moja ya magari ya yanayobeba mafuta

Nani kasema Mbagala mbele ya Nyumba Jalala, Angalia mandhari mazuri ya njia ya kuelekea Mbagala kama ilivyopigwa mchana wa leo

Sasa huyu hata sijui alikuwa anafanya nini mpaka ajali kama hii ikatokea...!!

Huu ndiyo muonekano mpya wa magari ya kubebea wanafunzi Jijini kama ilivyotangazwa na Halmashauri ya Jiji... safi sana yanavutia na pia ubebaji wa abiria ambao hawaruhusiwi kupanda gari hizo utakuwa umefikia kikomo.

Ni siku za hivi karibuni tu hii barabara imetoka kwenye ukarabati wa hali ya juu kabisa uliotumia fedha nyingi sana, lakini leo hii ukipata barabara hii ya Chang'ombe haitamaniki kutokana na mashimo kama haya.

Katikati ya barabara jamaa wese limekata...!
Page 1 of 8 pages 1 2 3 > Last » |