Home |
Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather |
|
Uzalendo
In this section you can find out the latest news and gossip in Bongo, the hottest music videos from your favorite artists and from a few up and coming acts, what celebrities got up to while they were at school, the latest street words, and what's happening in your favorite soap opera. UzalendoSuluhisho la UFISADI ni Nini?
Tatizo la Rushwa na UFISADI...
![]() Tatizo la Rushwa na Ufisadi limekuwa sugu kiasi cha kupelekea nchi yetu kuwa katika wakati mgumu. Tatizo hili limesababisha kuzorota kwa maendeleo ya nchi na kuleta malumbano baina ya wananchi na Serikali. Vyombo vya habari vimesadia katika kuonyesha na kueleza wananchi juu ya matatizo yanayokabili Serikali kutokana na athari za KIFISADI. Taarifa hizi zimeupa mwamko Jamii kwa kuielewesha maana ya UFISADI, athari zake katika jamii, pamoja na kuionyesha ni jinsi gani Serikali inapambana na tatizo hili. Kutokana na Elimu hiyo, wananchi wamepata muono wa jinsi gani ya kuwajibisha viongozi wao pamoja na kubaini haki zao katika utendaji wa Serikali kitu ambacho kimeonyesha ukuaji wa Demokrasia ya nchi, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na Mwananchi kutambua haki yake. Taarifa hizi zimepelekea wananchi kukosa imani na viongozi wao pamoja na kuwalaumu katika kutafuta suluhisho. Je suala la UFISADI ni tatizo linalosababishwa na Serikali ama wananchi kwa ujumla? Suala la UFISADI linahusisha watu wawili ama pande mbili kwa mtoaji (Mwananchi) na mpokeaji (Mtumishi wa Umma). Je, kuiwajibisha Serikali pekee katika mapambano dhidi ya UFISADI ndio suluhisho? Je suluhisho sahihi la UFISADI ni lipi? Mtoaji (Mwananchi) kuacha kutoa RUSHWA au mpokeaji kuacha kupokea (Mtumishi wa Umma) . Serikali ni Wananchi na Wananchi ni Serikali hivyo basi kwa mantiki hiyo vita ya UFISADI ni ya Wananchi wote kwa ujumla. Je kila Mwananchi akiwa Mzalendo, FISADI atatokea wapi? Tunaomba maoni yako Juu ya Janga hili lililoikumba jamii yetu kwa kupitia () PhotosMore on UzalendoReviewsComment Preview ![]() |
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: