Home |
Partly Cloudy and 25 C Dar-es-Salaam weather |
|
Uzalendo
In this section you can find out the latest news and gossip in Bongo, the hottest music videos from your favorite artists and from a few up and coming acts, what celebrities got up to while they were at school, the latest street words, and what's happening in your favorite soap opera. UzalendoUzalendo ni nini ?
Uzalendo ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele.
Uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno UZALENDO ni kubwa.
Elimu ya uzalendo ni elimu ambayo imekosekana kwenye jamii yetu. Hili linatokana na watu kutofundishwa kuipenda nchi yao. Upungufu huo ndio ambao hupelekea watu mbalimbali katika jamii kutenda mambo ambayo hushangaza watu na kuacha wengi katika mfadhaiko wa kujiuliza kama huyu mtu anaipenda nchi yake ama la.
![]() Uzalendo ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele. Uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno UZALENDO ni kubwa. Elimu ya uzalendo ni elimu ambayo imekosekana kwenye jamii yetu. Hili linatokana na watu kutofundishwa kuipenda nchi yao. Upungufu huo ndio ambao hupelekea watu mbalimbali katika jamii kutenda mambo ambayo hushangaza watu na kuacha wengi katika mfadhaiko wa kujiuliza kama huyu mtu anaipenda nchi yake ama la. Vitendo kama vya utoaji rushwa, upokeaji rushwa, upoteaji wa tamaduni (kutothamini kabila lako na chanzo chake), kutojiamini kama Mtanzania kwamba wewe ni bora kama wengine, wivu wa maendeleo uliyojikita kwa Mtanzania mwenzako na sio kwa mtu wa taifa lingine, kutothamini cha kwako na kutukuza cha mwenzako (Bidhaa za Tanzania, lugha ya Kiswahili, timu za mpira wa Ulaya) na kutojua ya kwamba utunzaji wa maslahi ya taifa lako ni jukumu lako na langu pia na sio la serikali pekee.. Kutokana na ukosefu wa elimu ya Uzalendo ambao unaleta madhara katika jamii mfano : kudumaa kwa maendeleo ya nchi yetu Dar411 imeona umuhimu wa suala hili kama chachu ya maendeleo ya nchi yetu na hivyo kuamua kulileta kwako wewe Mtanzania mwenzetu ili kutusaidia kutoa elimu hii ya uzalendo kwa jamii yetu ya Tanzania. Ukosekanaji wa elimu ya uzalendo umeleta athari kubwa katika jamii yetu na bila ya kupatiwa ufumbuzi litakuwa na athari kubwa zaidi kwa taifa la kesho.
Dar411 inakuomba wewe kama Mtanzania, utoe maoni yako, ya jinsi tutakavyoweza kutoa elimu ya uzalendo kwa kupitia tovuti hii ili kulisaidia taifa la kesho. Tunaomba ututumie maoni yako kwa kupitia anuani pepe yetu, ()
PhotosMore on UzalendoReviewsComment Preview ![]() |
Remember my personal informationNotify me of follow-up comments?
Submit the word you see below: